Maartje Eyskens and Francesc Campoy are organizing the fourth edition of the Go Devroom. Check out the following blog post for more information about CfP and how to get involved. In case you missed…
SOMO.
Mida ya saa mbili asubuhi nikiwa naelekea kwenye bomba la maji, mkononi nna chupa tupu ya maji, nahisi uchovu tena wa kuumwa kabisa ni kama nna malaria; nikiwa nimeamua kurejea nyumbani asubuhi hiyo hiyo, mwendo wangu ulikuwa ni wa kukubali kushindwa na hiyo hali na hivyo basi kuamua kwa hiari yangu kabisa kwamba vipindi vya siku hiyo sitahudhuria.
Nikiwa nalikaribia bomba la maji jirani na kantini nikakutana na Miriam (huyu ni dada nnaesoma nae) akaniuliza "unaenda kunywa chai?" Nikamjibu "hapana, naenda bombani", akaendelea "chai ushakunywa au utakunywa baadae?" Nikamjibu "sitakunywa asee, maana nataka nisepe", kwa mshangao akauliza "unataka usepe?! Kwanini wakati siku ndio imeanza?" Nikamwambia "sijiskii vizuri tangu usiku wa kuamkia leo nahisi ni kama nna malaria vile, so nachota maji ili nisepe home nikafanye mpango wa kupima afya, ila yule dada akasisitiza ninywe kwanza chai kama vipi kisha nisepe, ila sikuwa na salio la kutosha so nikamchana like "mafuta hayatoshi dada mkubwa", akaelewa na kunipa 5000 kisha akaniagiza ninywe chai alafu kiasi kitakachobaki nimrudishie.
Ile safari ya kwenda bombani niliikatisha na badala yake nikaenda kantini kuamsha. Kule nilikutana na mwanafunzi mwenzangu anaitwa David (sio jina lake halisi) nikamsalimia na nilimkuta ni kama anamalizia kunywa chai; basi mi nikaweka begi langu kitini kisha nikaenda kaunta kuagiza kifungua kinywa (chai, mhogo na kiazi), kisha nikaja nkaketi meza aliyokua ameketi nikamkaribisha huku nikijua kabisa hatakaribia, nilianza kugonga tea taratibu huku jamaa akiwa na simu janja yake kama kawaida yetu siku hizi, hahahaaa! Kisha akaanza kuongea na mazungumzo ndio niliyoanza nayo aya ya kwanza kabisa.
Ni kweli wiki iliyopita siku ya mwisho kuhudhuria mafunzo nilipiga mzinga wa nauli tena sio kwa mtu fulani, ila ni darasa zima nililitangazia na nilifanya hivyo nikiamini kabisa haitamshangaza mtu yeyote, tofauti na nilivyotarajia, ndugu David nilimshangaza, japo katika maongezi hakuonyesha ni kipi hasa kilichomshangaza na badala yake ukawa ni wasaa wa yeye kunisimulia changamoto aliyokutana nayo ambayo ndio hasa nimeamua niiweke hapa labda huenda ikawa ni chachu njema katika maisha yako ndugu. Karibu 😊
Jamaa anasimulia.
Siku unaomba hela nilikua nna jero tu kaka, na hata hiyo ilikuwa haitoshi kunifikisha napoishi ( jamaa anaishi Gomz na mahali tulipokuwa ni Mbezi beach), nilikua natamani sana nikuchangie chochote ila ndoivyo tena! Lakini hata hivyo ile siku nilikutana tu na muujiza asee, maana kwanza kabisa hakuna gari la moja kwa moja so ni lazima nikipanda hapa (Mbezi beach) lazima nishukie Mawasiliano kwanza, kisha nipande tena gari ya Gomz, maanake hapo nkwamba ile 500 itabaki 100 ila sasa kutoka hapo Mwasiliano hadi Gomzi ndio ishu (huyu mwana nadhani alikua anasonga kwa imani tu, na pengine labda alipanga tu kumuomba konda lifti, uzuri nkwamba nae ni mtu wa rohoni so itakua anaamini katika nguvu ya maombi).
Anaendelea kusimulia.
"Nilipofika Mawasiliano ile nashuka tu garini nikakutana na jamaa yangu nnaefahamiana nae kitambo na nilikua sjaonana nae kitambo ( hapo jamaa ana 100 mfukoni), nikasalimiana nae kwa furaha sana kisha akanisisitiza tukatulie sehemu tupate chakula huku tukipiga stori maana ni kitambo sana, ila kwa sababu na mimi sikuwa kwenye mood ya kutulia maana mawazo yalikua ni mengi usipime, so nilimwambia kama vipi nitakula mbele ya safari ila kuna sehemu nawahi so yule jamaa akanipa 5000, ni kama zali tu kaka, hebu na wewe fikiria."
Nilimuuliza kuhusu familia yake nikidhani wote wanaishi Dar ila alichonijibu ni kwamba ye ni mwenyeji wa Dom na hapa anaegesha tu, sa hapa sikutaka kumuuliza sana kama ni kwa ndugu ama niaje, maana kuna maswali mengine ukijibiwa ni muhimu upate full picture.
Akiwa Dodoma David alifanikiwa kuwa na biashara yake, na akafanikiwa kujenga hadi na nyumba mbili na akawa anajiwekea akiba kiasi kwamba akawa na akiba ya kutosha kujiendeleza zaidi.
Kipindi chote hicho jamaa aliendelea kubaki kuwa muumini mzuri msabato na akawa anajishughulisha na mambo kadha wa kadha katika kanisa alilokua akiabudia na katika utendaji wake kuna mmoja wa waumini alipendekeza kwa uongozi wa juu wa kanisa ndugu David ikiwezekana akasomee uchungaji kwa udhamini wa kanisa. Uongozi husika ulilipokea pendekezo hilo na kiukweli walimtia moyo na kumhakikishia kwamba watamsapoti kwa hilo.
Siku hazigandi, baada ya David kutafuta chuo na kufanikiwa alipeleka taarifa kamili kanisani, japo katika simulizi yake hakunitajia gharama, ila uongozi wa kanisa uliipokea hiyo taarifa na kuielewa kisha akataarifiwa kama kuna namna anaweza akapata udhamini kwa mwaka wa kwanza basi aende chuo kisha akirudi hizo gharama kanisa litalipia. Kutokana na bidii yake ya kuwa muwekaji wa akiba, David alifanikiwa kuwa na kiasi cha kutosha kumsomesha hata miaka miwili, hivyo aliamua kujilipia mwaka huo wa kwanza ila hakuutarifu uongozi wa kanisa kwamba pesa aliyolipa ilikuwa ni ya kwake mwenyewe, so alifanikiwa kwenda chuo kuanza mwaka wa kwanza na kule alienda kusomea kozi ya uchungaji na chuo alichopata kilikua Uganda. Kozi ilikuwa ni ya miaka mitatu. Sikumuuliza jina la chuo husika.
Mwaka wa kwanza ulipoisha alirudi Tanzania na kutoa ripoti ya maendeleo ya masomo yake lakini pia akaukumbushia uongozi kwamba, muhula unaofuata itabidi ufanyike utaratibu ili ipatikane pesa ya huo mwaka wa pili na pia lile deni la mwaka wa kwanza lilipwe. Uongozi ulimuelewa lakini ukatoa jibu kwamba kama bado kuna namna ya kupata msaada kwingine tena litakua jambo jema kwa sababu hata sasa (wakati huo yani) bado hali kiuchumi sio nzuri kutokana na muingiliano wa majukumu ya kikanisa, ila bado David aliahidiwa hiyo hela yote yaani ya mwaka wa kwanza na wa pili italipwa lakini pia kanisa litamlipia na mwaka wa mwisho likishalipa hayo madeni ya mwaka wa kwanza na wa pili. Jamaa akaona sio kesi.
Baada ya kuchungulia tena akiba yake akaona bado hata huo mwaka wa pili anaweza kujilipia gharama zote, akafanya hivyo, akaenda tena chuo kuendelea na masomo yake ya uchungaji kwa mwaka wa pili. Aliendelea vizuri na kama kawaida siku zinasonga, mwaka wa pili nao ukaisha akarudi nyumbani ajili ya kujiandaa na mwaka wa tatu.
Akiamini bado kanisa liko nae, alitoa taarifa ya maendeleo yake kama kawaida na kuwakumbusha hitaji walilonalo (kanisa) na kwamba umebaki mwaka mmoja hivyo basi waendelee kujipanga ajili ya kumsapoti kwa mwaka uliobaki na pia kulipa yale madeni ya mwaka wa kwanza na wa pili. Hakupata jibu la uhakika.
Siku za kufungua chuo zilivyokaribia zaidi huku kukiwa bado kuna ukimya wa uongozi wa kanisa, David aliamua kuulizia kinachoendelea na hapo ndipo alipojibiwa kwamba kanisa halikuwa bado na uwezo wa kumdhamini jamaa na hivyo basi kama anaweza kufanya namna mbadala ili aendelee kimpango wake afanye hivyo tu. David alishtuka sana, aliumia na akaanza kuwa na mawazo mengi sana kwani alihisi ni sawa kabisa na kutupa ile akiba yote aliyokuwa amejiwekea na kuamua kuitumia kujilipia elimu ambayo ingemfaa kutokana na wito wake na pia kutokana na ahadi ya kudhaminiwa na kanisa kama ulivyosoma hapa.
Wakati anaanza kusoma aliamua ile biashara aliyokuwa nayo (duka) aikabidhi kwa ndugu zake lakini mtu mmoja ndie aliyekua muuzaji ila hao wengine walikua ndio wasimamizi na wafuatiliaji wa mauzo na kwamba walikubaliana kila mwezi ndugu zake hao wawe wanamuwekea kwenye akaunti yake ya benki shilingi elfu hamsini kila mwezi ili awe anaendelea kujitunzia akiba kwa matumizi yajayo. Hakuwahi kuwekewa hiyo hela, na kadri siku zilivyokuwa zikienda ndivyo hilo duka lilivyofirisika.
Hakuwahi kuwa na mawazo mengi yenye kutawaliwa na utata wakati mwingine wowote kabla ya wakati huo, alishindwa aanzie wapi, hakujua amkimbilie nani, amlilie nani... Suala la kuendelea na biashara yake ambayo ilikuwa haiendelei tena japo kuna vitu vichache sana vya kuuza vilibaki ila navyo havikuwa na soko sana eneo lile na ndio maana ndivyo vilivyobaki. Alifikiria kuomba hata mkopo kwa wafanyabiashara wenzake ambao walikua wanaendelea na biashara zao vizuri na hao ndio alikua akifanya nao mishe za biashara kabla hajaamua kwenda kusoma, ili kama vipi afufue hiyo biashara yake akomae nayo tena. Nao walimtolea nje. Pia alienda kwa kaka yake mkubwa ajili ya kupata mkopo hata kwa kuweka bondi moja ya nyumba yake (hasa ile ya mwanzo) lakini nae akamjibu "katika vitu ulivyokosea mdogo wangu ni suala la wewe kwenda kusoma" huyo aliyemjibu hivyo ni mtu mwenye watoto na anawasomesha vizuri tena shule binafsi za kisasa.
Hakuna aliyejitokeza kukidhi haja za uhitaji wake alipotoa mapendekezo ya kuwezeshwa katika kufufua biashara yake ili angalau aendelee nayo maana uwezekano wa kurejea chuo ulikosekana kabisa na hata kanisa lake halikuwa na muda nae japo pamoja na hayo yote bado aliendelea kuwa muumini wa kanisa hilo.
Kufupisha stori hii ni kwamba jamaa nimekutana nae Dar akiwa ametokea Dodoma, na hapa yupo ajili ya mafunzo ya matumizi ya sauti kwa watangazaji wa TV na redio, pamoja na wasanii waigizaji wa filamu na wanamuziki, ila yeye ni sehemu ya wanamuziki waimbaji na nilibahatika kusikiliza demo ya kazi yake moja. Hajakata tamaa na bado anaamini kwamba uwezekano wa kufikia malengo yake (mafanikio) bado ni mkubwa.
Alikatisha masomo yake ya chuo ambayo ulibaki mwaka mmoja tu ahitimu. Kanisa lililoahidi kumsapoti kama ulivyosoma ni kama lilimgeuka, ndugu zake aliowakabidhi biashara yake waiendeleze nao wakashindwa kuiendeleza, wafanya biashara wenzie pia wakashindwa kumkopesha na tena aliwapa mazingira ya namna atakavyokuwa anawalipa wakamtosa hata mkopo wenye riba, kaka yake nae alitosa kumkopesha pesa tena kwa kumuomba ashike moja ya nyumba zake kama bondi. Hayo yote alikutana nayo baada ya kua ametumia akiba yake kujilipia gharama za elimu ya chuo kikuu alikokua anasomea uchungaji, kwa nguvu ya baraka za uongozi wa kanisa za kumsapoti jamaa tena kwa ahadi ya kumlipia na kulipa gharama zilizohusika katika elimu yake hata kama alikopa kwingine. Najaribu kijiuliza kama angekua kweli hizo pesa amekopa kwa watu saivi hali ingekuaje?! Anyways, hii yote ni namna ya kujifunza kutokana na mapito.
Kuna mengi sijayaweka hapa ila yatakuwa sehemu ya kitabu changu nachoendelea kukiandika sasa. Ishu ni kwamba kila mtu ana jambo ambalo bila shaka linaweza kuwa funzo kubwa sana kwako, na hii inamaanisha kwamba ni muhimu sana kupeana masikio ili kwa shuhuda zetu wenyewe na za wenzetu tujifunze na kuwafunza wengine.
Ndugu David (sio jina lake) kanifundisha mengi sana kiasi kwamba nachelea kumuamini kila mtu katika maisha haya hata awe papa, hell no!
Unaweza ukaamua mwenyewe ni kipi umejifunza kwa haya machache. Asante.
When it comes to security cameras, there are many brands available in the market, and each has its strengths and weaknesses. However, some brands stand out for their reliability, features, and…
Now that the age of Instagram is upon us, having Photoshop skills can drastically improve your online presence. You might be looking for a way to edit the photos that you have taken or considering a…
Having high-performing landing pages is essential for both start-ups and well-established firms for enhancing their business growth. Important for strengthing their inbound marketing strategy…